16 June 2018 ni Siku ya mtoto wa Africa: Nchi yatu Tanzania kama sehemu
16 June 2018 ni Siku ya mtoto wa Africa: Nchi yatu Tanzania kama sehemu ya Africa inaelekea kwenye Uchumi wa Viwanda na wa Kati, Tunapaswa kuzijua mbinu za kufika huko
Unapomfuata mwenye Kiwanda au tekinologia kumtaka kushirikiana naye SWALI LA KWANZA ATAKALOKUULIZA NI HILI: Je wewe una nini?. Jibu: Nina BRAND na mtaji JAMII/SOKO. Kwa nchi zilizoendelea silaha yao kubwa ya maendeleo ni FEDHA, lakini sikutaja FEDHA kwa sababu kwa kuzingatia hali ya uchumi wetu hatuwezi kutumia FEDHA kama msingi wa maendeleo kwa sababu FEDHA tuliyonayo ni kidogo mno. ILA KAMA unamiliki BRAND na mtaji JAMII, wenye FEDHA na tekinologia watakusikiliza kwa sababu wao wana FEDHA lakini SOKO ni changamoto kwao. Mtu atajiuliza mfano wa BRAND ni upi? Mfano ni tHL: Brand hii ya tHL ni ya hapa Tanzania, sasa ina nguvu ya kuzungumza na wenye viwanda kuzalisha bidhaa za thl kama simu, tablets, computer, n.k. Na tuna nguvu ya kushawishi viwanda kuja kuwekeza hapa nchini wakishajiridhisha upande wa SOKO. Nguvu ya tHL sio FEDHA ni JINA(BRAND) na WATU wanaoiunga mkono, na vitu hivyo ndo vinasukuma wawekezaji kushirikiana nasi na wengine wakitaka wenyewe bila kuwaomba. Narejea azimio la Arusha: Maendeleo ya nchi huletwa na watu, hayaletwi na fedha. Fedha ni matokeo siyo msingi wa maendeleo. Mada hii ni Pana nitajitahidi siku zijazo kuleta ufafanuzi wa kina kuhusu MBINU ZA KUANZISHA BIASHARA ZA KIMATAIFA NA VIWANDA. Jacob Noel Urasa. One Love See more