Elimu ya Msingi(Primary) ni miaka SABA(Darasa la Kwanza mpaka la Saba)
Elimu ya Msingi(Primary) ni miaka SABA(Darasa la Kwanza mpaka la Saba) NA watoto hawataishia darasa la SITA. Mitaala inayopaswa kutumika ni ya miaka saba. UFAFANUZI huu umetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na teknolojia Prof Ndalichako bungeni tarehe 13 June 2018, amesema hakuna waraka wowote uliotolewa ambao Elimu ya msingi ni Miaka sita na sheria ya elimu inayotumika ni ya mwaka 1978 na haijabadilika, sheria hii inaonyesha elimu ya msingi ni miaka saba.